SILVERLANDS_LOGO_FULL-COLOUR_WEB copy.pn

SISI NI NANI?

Silverlands ilianzishwa mwaka 2013 kuhudumia soko linalokua kwa kasi la uhitaji wa bidhaa bora za kuku hapa Tanzania. Kukua kwa STL ni uthibitisho wa uthabiti wake katika ubora wa bidhaa na bei nafuu.
Kampuni ya STL inalenga kuzalisha vifaranga bora na chakula kwa ajili ya wakulima wa ndani ili kuhakikisha wanafanikiwa. STL inazalisha vifaranga vya kuku wa aina mbalimbali wanaofaa katika masoko yenye uhitaji tofauti. Hii inawapa wateja wetu fursa ya kuchagua aina ya kuku inayofaa kwa mazingira yao. Aina zote za kuku wa STL wa nyama na wa mayai, wamechaguliwa kutokana na uwiano mzuri wa vigezo vya tabia mbalimbali na ufanisi wake katika ufugaji, hii pia itasaidia kama kutakua na usimamizi mzuri.


Hatua hii ina hakikisha kuku wanamatokeo ya viwango vya juu kabisa katika mazingira tofauti ya ufugaji.

Bidhaa

STL tunajivunia uzalishaji wa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na bei nafuu sana kwa wafugaji

 Umakini katika kuhakikisha ubora ni muhimu sana, tuna miundo mbinu inayotuwezesha kuzaliza bidhaa ambazo zinaubora tunaoamini ni zaidi ya viwango vinavyokubalika katika soko la ndani na la nje ya nchi.

Malighafi

Kwa kua STL ina maghala yaliyosajiliwa na bodi ya stakabadhi ghalani, ili mahindi yaweze kupokelewa na STL lazima yafikie viwango vya ubora wa mahindi vya Jumuia ya Afrika Mashariki. Kimsingi, kigezo kikubwa zaidi cha ubora ni kiwango cha unyevu ambacho kinapaswa kisizidi 13.0%. Mahindi yote na maharage ya soya yanayopokelewa yanapimwa katika maabara ya STL kwa kutumia machine ya NIR kuthibitisha viwango vya virutubishi kabla ya kutumika.
Wakulima wote wanaopenda kuuza mahindi yao kwa STL, tafadhali wasiliana na maneja manununzi wa STL

Washirika wetu

Silverlands-PTC-logo.png

Technical Poultry Education Centre

Silverstreet.jpg

SilverStreet Capital

Ross.jpg

Ross

CEVA.jpg

Ceva

hy line.jpg

Hy-Line

Sasso.jpg

SASSO

WPF.jpg

World Poultry Foundation