Mafanikio ya kiwango chochote katika ufugaji wa kuku wa nyama yanategemea sana mafanikio katika utunzaji wa kila siku katika nyanja zote za maisha yao.

Kati ya nyanja zote za utunzaji zinazohitajika ili kukuza kuku wa nyama kwa mafanikio, chakula kina athari kubwa kuliko zote. Chakula kinachukua takriban 65% mpaka 70% ya gharama zote za uzalishaji wa nyama ya kuku.

Kwahiyo, ni muhimu kuhakikisha chakula kipo sawa katika nyanja zote za ubora na udhibiti wa chakula kulingana na mfumo wa ulishaji unaotumiwa, wakati wote upo sawa ili kuhakikisha uwezo wa ukuaji wa haraka walionao kuku unatoa matokeo hayo ya kuku kukua haraka iwezekanavyo.

 

Kama chakula chetu kikitumiwa kukuza kuku wa nyama wa Silverlands inawezekana kupata uwito wa 1.4kg baada ya siku 28 na ufanisi wa chakula kwa uzito wa kiwango (FCR) cha 1.4.

 

Kwa ufanisi wa juu kabisa uwezekanao wa ukuaji, tunashauri mpangilio wa ulishaji wa chakula kama ifuatavyo:

  • Silverlands Broiler Pre-Starter Crumble - Siku 0 mpaka 7

  • Silverlands Broiler Starter Crumble – Siku 8 mpaka 14

  • Silverlands Broiler Grower Pellet – Siku 15 mpaka 27

  • Silverlands Broiler Finisher Pellet – Siku 28 mpaka 42

Chakula cha kuku wa Nyama