Chakula cha kuku wa mayai

Kuku wa kisasa wa mayai wana vinasaba vya uwezo wa kuanza kutaga mapema, kuwa na ufanisi mkubwa wa `chakula kwa ukuaji` (FCR) na matokea ya viwango vizuri vya utagaji wa mayai.

Japokua lengo kuu la mfugaji wa kuku wa mayai ni kupata mayai mengi na mfululizo, hatua za mwanzo za ukuaji wa kuku nazo ni muhimu sana. Kwahiyo ni muhimu kuhakikisha kiwango bora cha utunzaji wa kuku katika nyanja zote tangu siku ya kwanza. Kati ya nyanja za utunzaji wa kuku zilizo muhimu sana ni chakula. Gharama za chakula ni takriban 65% mpaka 70% ya gharama zote za utunzaji wa kuku wa mayai.

vyakula bora vya kuku tunavyozalisha vinahakikisha lishe sahihi kwa ustawi wa kuku katika ngazi zote za ukuaji

Mpangilio wetu wa vyakula vya kuku wa mayai upo katika ngazi nne:

  • Silverlands Broiler Starter Crumble-Siku 0 mpaka siku 13

  • Silverlands Layer Starter Mash- Siku 14 mpaka siku 42

  • Silverlands Grower Mash- Siku 43 mpaka siku 126

  • Silverlands Complete Layer Mash-kuanzia siku 127 mpaka kuku watakapo uzwa baada ya kutolewa katika utagaji.