STL ni kampuni inayoongoza katika uzalishaji wa chakula cha kuku Tanzania na inahitaji mahindi na maharage ya soya yenye ubora wa hali ya juu
Kampuni ina miundo mbinu ya kuhifadhia nafaka yenye uwezo wa tani 32,000 katika makao yake ya Makota. Kampuni ina nia ya kuwa soko la mahindi na maharage ya soya kwa wakulima wadogo wadogo
STL pia imesajiliwa na mamlaka ya maghala Tanzania na inaweza kuwahifadhia wakulima mahindi katika vihenge vyake
Ubora ni moja ya nguzo muhimu za STL, kwahiyo malighafi zinazopokelewa zinapitia uchunguzi mkali wa ubora kabla ya kukubalika