KITUO CHA MAUZO SINGIDA

Mwonekano wa mwisho wa kituo cha mauzo Singida.

 

Hiki ni moja ya kituo kipya cha Silverlands cha  usambazaji wa bidhaa zetu kwa kanda ya kati kilichopo eneo la Kibaoni katika barabara inayokwenda Mwanza mjini Singida.

 MATANGAZO RADIONI MTWARA

Mwezi wa Nne, 2021 

Katika kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wafugaji wetu pamoja na kuwapa elimu juu ya ufugaji bora, Timu ya Masoko Silverlands pamoja na Meneja mauzo Mkoani Mtwara, imefanya ziara radioni mkoani humo kwa lengo la kutoa elimu juu ya bidhaa na huduma bora zitolewazo na Silverlands Tanzania.

Kuweza kusaidia wateja wetu kufahamu upatikanaji wa bidhaa zetu kiurahisi katika Mkoa wa Mtwara na wilaya zake.

Kwenye Kipindi cha radio tumeweza kuwaelimisha wasikilizaji juu ya vifaranga bora na chakula bora kinachozalishwa na Silverlands, Huduma ya mafunzo ya ufugaji bora wa kuku inayotolewa na Silverlands kupitia chuo chake kinachoitwa

PTC(Poultry Training Centre),

pamoja na huduma ya maabara(SDL) kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo.

Kupitia simu pamoja na jumbe fupi za maandishi kutoka kwa wasikilizaji tumeweza kutatua changamoto na kutambua wauzaji halali wa bidhaa za Silverlands katika wilaya za mtwara na maeneo jirani.

Matangazo yetu yameweza kuwafikia wasikilizaji wa Mtwara na wilaya zake, Masasi,Tandahimba mpaka Tunduru.

SEMINAR NA MIKUTANO YA UHAMASISHAJI DODOMA.

Mwezi wa Tatu, 2021 

098fa90e-d292-4351-aa06-2b15b51cde8c.jpg
IMG_8552.heic

Semina na mikutano ya uhamasishaji husaidia kuwafikia  wafugaji wa kuku, Pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili.

 

Walengwa wa mikutano ya uhamasishaji ni wafugaji wote wa kuku  na wale wasio wafugaji

 

Wafugaji wadogo hunufaika sana kutokana na uhamasishaji, hupata majibu ya maswali yao kuhusiana na ufugaji wa kuku.

Katika kuwasaidia hawa wafugaji wadogo, huwa tunatoa elimu juu ya ufugaji bora wa kuku na kufuga kibiashara, Tunawasaidia kwa kuweza kuwapa elimu ya ufugaji kwa kuanza na mtaji mdogo na baadae kuweza kukumiliki kuku wengi Zaidi.

 

Kuku aina ya sasso wameweza kusaidia kaya nyingi kwa kuongeza kipato kupitia ufugaji wa kuku kama biashara, pia husaidia familia  nyingi kuimarisha lishe kupitia ulaji wa nyama ya kuku Pamoja na mayai.

 

Semina na Mikutano ya uhamasishaji iliyofanyika Dodoma imesaidia kuongeza ufahamu kwa wateja wetu juu ya bidhaa zinazopatikana Silverlands Pamoja na huduma zitolewazo.

Katika huduma zitolewazo Silverlands ni  mafunzo ya ufugaji bora wa kuku kutoka katika chuo chetu (PTC) Pamoja na Maabara nzuri na ya Kisasa inayoweza pima magonjwa ya kuku na kutoa ushauri.

MIKUTANO YA UHAMASISHAJI KANDA YA ZIWA.

Mwezi wa Pili, 2021 

     Mwanzoni mwa Februari Timu ya Masoko imefanya Semina na mikutano ya uhamasishaji katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na wilaya zake lengo ni kuongeza uelewa juu ya lishe bora kwa kula nyama ya kuku Pamoja na mayai na kuongeza mapato kupitia ufugaji wa Kuku kibiashara, Pia kumsaidia mwanamke kuweza kumiliki biashara kupitia ufugaji wa kuku.

Kwa kushirikiana na mshauri wa Shirika la Kuku Duniani tumesaidia kuongeza uelewa juu ya masuala ya jinsia na lishe katika familia na jamii kwa ujumla.

 

     Kuku ni chanzo kizuri cha protini na lishe bora, na ana faida nyingi kiafya. Sasso ni  kuku wa kienyeji aliyeboreshwa, Sasso ni kuku wa nyama Pamoja na mayai, Ni Kuku anayekua haraka ikilinganishwa na kuku wa kienyeji, anataga mayai mengi hadi 240 katika wiki 72, Mwenye kustahimili  magonjwa na vile vile  hatumii dawa yoyote ili aweze kukua.

Pamoja na usimamizi mzuri kutoka kwa Kitengo  Mama , Sasso anafikia hadi uzito kati ya  gramu 700 hadi  gramu 750 , Hii humsaidia Kitengo Mama  kumuza sasso wa mwezi mmoja kwa Shilingi 5000/=

 

      Katika miezi 2.5 Sasso anaweza kufikia uzito wa 2kg hadi 2.5kg na kuuzwa hadi TZS 15,000 /

      Mfugaji wa kuku  aliyefanikiwa lazima awe na ustadi na maarifa juu ya usimamizi bora wa Kuku, Usalama wao, Pamoja na chanjo.

 

     Kituo chetu cha Mafunzo ya Kuku huko Makota kimekuwa msaada mkubwa kwa wafugaji wengi kufanikiwa sana juu ya ufugaji wa kuku kupitia ujuzi mzuri wa mafunzo na kozi zitolewazo hapo

 

     Silverlands kupitia mpango wa APMI, Timu yetu ya masoko imehamasisha katika wilaya ambazo ambazo wapo kikazi. Wilaya hizi ni Magu, Kwimba, Misungwi na Sengerema huko Mwanza, Chato, Mbogwe na Nyang’hwale, huko Geita na Kwa Mkoani Shinyanga ni Kahama na Wilaya ya Shinyanga.

 

      Uhamasishaji unasaidia kuzisikia changamoto za wafugaji na kuwapa ushauri na mbinu za ufugaji bora na wenye tija.

UZINDUZI WA MUONGOZO WA UWEKEZAJI

Mwezi wa Kwanza, Tarehe 23, 2021 

       Uzinduzi wa Mwongozo wa uwekezaji mkoa wa Iringa ulifanyika katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Mkwawa, Ukiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh Kassimu Majaliwa Majaliwa. Tukio hilo liliambatana na uwasilishaji wa  fursa zinazopatikana ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kuonyesha Maono ya Mkoa wa Iringa. Uzinduzi huo uliwaalika wakezaji kutoka Iringa, Silverlands Tanzania ikiwa Mwakilishi.

   

      Tukio lilianza kwa Majadiliano yaliongozwa na Waziri wa Uwezekaji ofisi ya Rais Mh Prof. Kitila Mkumbo ikiambatana na uzinduzi wa uliongozwa na Waziri mkuu. Kufatia uzinduzi huo kulikuwa na Maonyesho ya kuonyesha bidhaa, huduma zilizoletwa na Wawekezaji wa Mkoa wa Iringa.

   

      Silverlands Tanzania ilionyesha chakula bora cha kuku na Vifaranga wa siku moja wanaozalishwa Iringa, na  wanapatikana nchi nzima.

Pia Silverlands ilionyesha vifaa  na uwezo wa kufanya uchunguzi kwenye magonjwa ya wanyama kwa kupitia Kituo cha Mafunzo ya Kuku na Maabara ya Uchunguzi ya Silverlands.


     Silverlands ilionyesha kuku wa kuchoma ili kuwapa nafasi washiriki ya kuonja radha ya kuku aina ya SASSO na kujadili umuhimu wa SASSO katika kuboresha lishe.

KUTEMBELEWA NA UBALOZI WA UINGEREZA

Mwezi wa Kwanza, Tarehe 22, 2021

      Silverlands Tanzania walipata nafasi ya Kumkaribisha Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mh David Concar Shambani, Makota akiambatana na Mkuu Wa Wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela.

Hii fursa iliwapa nafasi Silverlands kuomyesha wageni mbalimbali mbinu za ufugaji wa kuku kitalaamu, na Namna jamii vijijini wanavyoweza kufaidika kupitia ufugaji wa kuku.

      Mr. David Concar aliandika katika ukurasa wake wa twitter akisema "Nimevutiwa na Silverlands Tanzania hasa wanavyowafikia na Mpango wa Mafunzo ambao unabadilisha maisha ya wanawake      katika jamii kwa kuwawezesha wao kufuga kuku wa kiwango bora  na kuuza kwa faida nzuri.

Habari njema kutoka Kenya

WPF na BMGF Watembelea wafugaji wadogo Morogoro

Wafanyakazi wa Silverlands wakiongozwa na Meneja wa Masoko Mwanamvua Ngocho. Katika Picha ya Pamoja na wageni kutoka Shirika la ndege wanaofugwa duniani.

World Poultry Foundation na Bill & Melinda Gates Foundation wakiwa na Kitengo Mama pamoja na wafugaji wadogo walioko chini ya mradi wa kuongeza kuku walioboreshwa Africa(APMI) Mjini Morogoro.

WPF na BMGF walipata muda wa kuwatembelea wafugaji wadogo pamoja na Kitengo Mama.

ili kuwezaa kujionea uboreshaji wa lishe katika kaya kwa kuongeza uzalishaji wa nyama ya kuku na mayai.

Wanatarajia kuona matokeo mazuri ya uzalishaji wa nyama na mayai ambayo yataliwa na familia haswa watoto wadogo.