Taarifa Zetu

Silverlands Tanzania Limited (STL) ilianza kwa uzalishaji wa vifaranga na chakula cha kuku mwaka 2014 kwa ajili ya wafugaji wakubwa na wadogo hapa Tanzania.

 

Makao yetu makuu na miundo mbinu ya uzalishaji ipo katika shamba la Makota, kijiji cha Ihemi, mkoa wa Iringa

 

Mwanzoni mwa 2017, miundo mbinu mipya ya uzalishaji chakula cha kuku pamoja na uhifadhi wa mali ghafi ilizinduliwa rasmi. Kiwanda hiki kipya chenye mifumo inayoendeshwa kwa udhibiti wa komputa, cha uzalisha wa chakula cha kuku kina uwezo wa kuzalisha tani 40 za chakula kwa saa.

Kwa pamoja, uwezo wa kuhifadhi tani 32,000 za mali ghafi na uwezo wa kuzalisha tani 40 kwa saa, unafanya Silverlands kuwa moja ya viwanda vikubwa zaidi katika Afrika Mashariki vya uzalishaji wa chakula cha kuku.

Kiwanda hiki kimewezesha kuimarika zaidi kwa ubora wa chakula na ufanisi wa uzalisha unaoifanya Silverlands kumudu kuwahudumia wateja wake ambao idadi yake inaongezeka kwa kasi.

 

      Kwa sasa, STL ndio kampuni pekee inayozalisha aina tatu tofauti za vifaranga na kuvisambaza katika soko la kuku hapa Tanzania.

STL inaingiza vifaranga vya kuku wazazi toka katika makampuni ya kuku wazazi yanayojulikana kimataifa kwa ubora, ili kuhakikisha wateja wake wanapata vifaranga vyenye ubora na ambavyo, kijenetiki vinakwenda na wakati na vinauwezo mkubwa wa kutoa matokeo mazuri.

STL imefanikiwa kupata hati ya makubaliano ya haki pekee  ya usamabzaji (Exclusive Distribution rights) hapa Tanzania wa kuku wa SASSO ambae anaweza kukuzwa kama kuku wa mayai au wa nyama na ni kuku anaekua polepole.

 

 

STL imeingia makubaliano ya ushirikiano na World Poultry Foundation (WPF) ambayo ni taasisi ya uendelezaji wa tasnia ya kuku duniani, kufanyia kazi mpango wake wa ukuzaji na usambazaji wa kuku hapa Tanzania, ujulikanao kama African Poultry Multiplication Initiative (APMI).

Katika mpango huu, kupitia usambazaji wa vifaranga vya kuku wa SASSO, STL itasambaza kwa wakulima na wafugaji wadogo, hasa wa vijijini, kuku walioboresha kijenetiki, itatoa msaada wa kitaalam pamoja na mafunzo kwa wafugaji hao wadogo, pamoja na kusaidia kufungua fursa za masoko ambazo hazikuwezekana hapo kabla.

Mpango huu utasaidia kukuza Ufugaji na kuongeza tija katika Ufugaji wa kuku, Kukuza kipato na lishe katika kaya pamoja na kuwainua kiuchumi kinamama.

 

 

Mtandao wetu wa usambazaji wa bidhaa zetu unakua kwa kasi.

Kwa sasa, kupitia mtandao wetu wa rejareja tunaweza kusambaza chakula na vifaranga vyenye ubora wa hali ya juu kwa wateja wetu wanaoongezeka kila leo nchi nzima.

 

 

Kwa kuamini katika mahusisno ya muda mrefu na wateja wetu, STL ilianzisha kituo cha mafunzo ya Ufugaji kuku 2016 (T-PEC), katika shamba lake la Makota, Ihemi. Malengo ya mafunzo yanayotolewa ni kuwafanya washiriki waweze kuendesha kwa mafanikio na tija vituo vya kukuzia kuku ama mashamba yao ya kuku.

Tunajali na kupenda sana kazi yetu, wateja wetu na mazingingira.